Press "Enter" to skip to content

Semina ya Wanamaria Parokia ya Mt. Karoli Lwanga, Muyeye, Malindi.

Semina ya Wanamaria ilifanyika katika Parokia ya Mt. Karoli Lwanga tarehe 13 Novemba 2026. Semina hiyo ililenga kuwajengea Wanamaria maarifa, maadili na moyo wa kumfuata Mama Maria katika maisha yao ya kila siku.

Semina ya Wanamaria – Parokia ya Mt. Karoli Lwanga

Mafundisho ya Madam Patricia – Dekania ya Watamu

Madam Patricia, ambaye amekuwa mwanamaria na mlezi kwa muda mrefu, aliwafundisha Wanamaria mambo mbalimbali, yakiwemo:

  1. Sherehe zote za Mama Maria na maana zake.
  2. Kanuni zote ishirini pamoja na maelezo kamili. Miongoni mwa kanuni hizo ni:
    · Kumfuata Bikira Maria, msimamizi wa wanachama, na kuzifuata nyayo zake.
    · Wanachama kufanya maungamo mara kwa mara.
    · Kuwatii wazazi wao.
    · Kufanya usafi kanisani.
    · Kuwa mfano mwema kwa wengine na mambo mengine.
  3. Muundo wa shirika, pamoja na vipengele vyake kumi na mbili, kama vile:
    · Uongozi wa shirika na majukumu yao.
    · Sakramenti kamili.

Aidha, Madam Patricia aliwahimiza Wanamaria kuhudhuria Misa kila siku inapowezekana, kuzingatia mavazi yanayofaa kanisani kama mwanachama, na kuelewa sheria na kanuni kabla ya kufanya uamuzi kamili wa kupokelewa.

Maelekezo ya Sr. Patricia – Coordinator wa Wanamaria

Sr. Patricia, coordinator wa Wanamaria, aliwakumbusha Wanamaria umuhimu wa kujiweka chini ya ulinzi wa Mama Maria wanapoendelea na masomo yao, ili wawe na uamuzi mzuri kuhusu wito wao. Pia aliwahimiza kujiweka safi kimwili, kiroho na kiakili.

Mama Sabina Musa – Mlezi wa Parokia ya Muyeye

Mama Sabina Musa, Mlezi wa Parokia ya Muyeye, aliwahimiza Wanamaria:

· Kuwa watoto watiifu, wenye heshima na wanaowavutia watoto wengine.
· Kupenda sala na kusaidia wazee, maskini na wagonjwa kwa sala, na kujitolea kuwatembelea.

Mama Alice – Mlezi wa Muyeye

Mama Alice, Mlezi wa Muyeye, aliwahimiza Wanamaria kuamua kusimama imara na kukataa marafiki wasio na mwenendo mzuri. Aliwataka kuwaombea watoto waliopotoka na kufanya bidii katika masomo, kanisani na nyumbani.

Fr. Damas – Chaplain wa Wanamaria katika parokia na Dekania ya Cathedral.

Fr. Damas, chaplain wao, aliwapa Wanamaria nafasi ya maungamo na kuwaongoza katika Misa. Aliwakumbusha kuweka mafundisho hayo moyoni, wakiomba msaada wa Mama Maria ili kuweza kuyatafakari na kuyafuata kama Wanamaria wa wakati huu.

Semina hiyo ilikuwa na tija kubwa, ikawapa Wanamaria hamasa ya kuendelea kukua katika imani, maadili na huduma kwa Kanisa na jamii

Copyright © 2026 Saint Charles Lwanga Muyeye | Backend: Mukulu SJ | Mission News Theme by Compete Themes.